Wakati Rais Magufuli akiendelea kujadiliwa kila kona ya dunia kutokana na maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya ndani ya siku 30 tangu amekuwa Rais, Kenya kuna stori ambayo iko tofauti kidogo kumhusu Rais Kenyatta na safari zake nje ya nchi.
Mitandaoni kuna picha inayoonesha bango linalomkaribisha Kenya Rais Kenyatta, limeandikwa hivi >>>> ‘KARIBU KENYA‘ <<<
Lakini hiyo ‘karibu’ yenyewe inawezekana isiwe na maana ya moja kwa moja kutokana na rekodi za safari za Rais huyo nje ya nchi ndani ya miaka mitatu ya Urais wake… rekodi zinaonesha Rais Kenyatta ameongoza kwa kusafiri nje ya nchi mara 43 ndani ya miaka mitatu kwenye Urais wakati Rais Mstaafu, Mwai Kibaki alisafiri mara 30 ndani ya miaka 10 ya Urais wake.
Safari ya mwisho ya Rais Kenyatta alienda South Africa na Ufaransa… Ripoti ya Serikali imesema japo wanaokosoa safari hizo ni wengi lakini bado kuna umuhimu Rais huyo kusafiri nje ya nchi mara kwa mara.
Video na stori yenyewe hii hapa kutoka kituo cha K24 TV ya Kenya.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.