Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka amefunguka kwenye exclusive interview na Ayo Tv amefunguka kuhusu kauli iliyowahi kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini ya kwamba amesema Milioni 10 za ESCRO zilikuwa ni pesa za mboga kwake.
“Sijawahi na huwezi kuleta clip niliyosema Bilion moja ni fedha ya mboga, mimi nilikuwa ninamjibu Mwanasheria wa Serikali nikiwa nimeshitakiwa katika Mahakama ya maadili baada ya kuniuliza Milion 10 hizi zilikuwa za nini kwenye Bank statement lakini unajua kwa sisi Wahaya huwa tunazungumza kwa kejeli”
“Ela ya mboga ni pesa ya matumizi ya kwangu binafsi, sasa walikuwa wameandaliwa Waandishi kwa ajili ya kunichafua lakini wakashindwa. Mimi ni mtu mzima na vitu vya kupita havinipi shida”- Prof. Anna Tibaijuka
PROF. TIBAIJUKA AFUNGUKA TUSIYOYAJUA KUHUSU DR. MENGI, UTATA WA KIFO CHAKE “NI UJINGA”