Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Leo December 28, 2017 imeidhinisha gawio la Tshs bilioni 300 kwa serikali kutokana na faida iliyopatikana kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Kiasi hicho kinafanya jumla ya gawio ambalo Benki Kuu ya Tanzania imetoa katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2014 kuwa Tshs bilioni 780 kwani mwaka 2014/2015 ilitoa gawio la Tsh bilion 180 na mwaka 2015/2016 gawio lilikuwa Tsh bilioni 300.
Kwa mujibu wa sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, jukumu la msingi la BoT ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.
UKAGUZI WA CAG: “UVCCM imeongoza kwa hesabu safi kati ya Jumuiya zote za CCM” – Katibu UVCCM