Kuna utofauti kwenye aina ya usafiri, uko usafiri wa umma ambao kila mtu anajilipia na anasafiri na upo usafiri binafsi, ukiwa kwenye usafiri wako binafsi unaenjoy tu vizuri na kujiachia, lakini ukiwa kwenye usafiri wa watu wengi inabidi kidogo uwe mpole.
Mtoto wa Bosi wa Shirika la ndege Korea amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kuvunja sheria za ushafirishaji wa anga baada ya kuamrisha ndege kusimamisha safari ili wahudumu wa kwenye ndege hiyo washushe.
Mtoto huyo alikasirishwa na kitendo cha wahudumu hao kumpatia macadamia nuts ambazo ziko kama karanga kwenye mfuko badala ya kuwekewa kwenye bakuli.
Mtoto huyo Cho Hyun-ah ambaye umri wake ni miaka 40 aliomba msamaha baada ya hukumu hiyo lakini mahakama haikumpunguzia adhabu.
Baba yake Cho Yang-ho naye alionekana kukasirishwa na kitendo hicho, huku watu wa Korea nao kukosoa zaidi tabia za watu hao wenye uwezo kifedha kuonekana mara nyingi wako juu ya sheria za nchi.
Msichana aliwahi kuwa
Ndege hiyo ilikuwa ikitokea New York Marekani kwenda Seoul, Korea Kusini.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook