Premier Bet
TMDA Ad

Duniani

Nchi ambayo bado TV ya taifa haijatangaza chochote kuhusu ushindi wa Trump

on

Unaweza kufikiri mpaka sasa dunia nzima inafahamu kuwa Donald Trump ndiye raisi mteule wa Marekani lakini sio hivyo sababu kwenye taifa la Korea Kaskazini bado vyombo vya habari vya taifa mpaka sasa havijatoa habari yoyote ya  ushindi wa Donald Trump kwenye Urais Marekani.

Mwandishi Chris Greenway wa BBC aliandika kwenye mtandao wa Twitter kwa kusema  Leo ni Jumatatu hapa Korea Kaskazini ambapo mpaka sasa vyombo vya habari vya taifa havijawataarifu Wananchi wake juu ya matokeo ya uchaguzi nchini Marekani.’

 

 

Inasemekana kwa Korea Kaskazini sio rahisi kwa vyombo vya habari vya taifa kufanya hivyo kwani taarifa huwa zinachujwa na Wananchi hupokea habari zile tu ambazo serikali imezipitisha na sio vinginevyo.

Kwenye uchaguzi wa safari hii Marekani kwa Korea Kaskazini umekua tofauti na ule wa 2008 ambao Korea Kaskazini ilitangaza matokeo yake siku tatu baada ya Barack Obama kushinda.

VIDEO: Uliikosa show ya DIAMOND PLATNUMZ iliyovunja rekodi Marekani? tazama hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments