Kila ifikapo May 3 dunia huadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ikiwa ni katika kuungana na wanahabari kwa kutambua haki, maslahi na ulinzi wao ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku hiyo.
Katika kuadhimisha siku hii Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kagera ‘KPC’ kimeadhimisha siku hii kwa kutembelea Shule ya Msingi Tumaini yenye wanafunzi wa mahitaji maalum.
Ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mbeki Mbeki, KPC kimetoa msaada kwa wanafunzi wenye mtindio wa ubongo – vifaa vya kufanyia usafi na kujifunzia madarasani.
Kaulimbiu ya mwaka huu kitaifa ni: “Fikira yakinifu, Jukumu la Vyombo vya Habari katika kudumisha Amani, Usawa na jamii Jumuishi” huku kaulimbiu ya Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania ‘UTPC’ ikiwa ni: “Klabu za Waandishi wa Habari nchini zihimize aman na shughuri za kijamii katika maeneo yao”.
VIDEO: Waandishi walioshambuliwa kwenye vurugu za CUF wasimulia. Bonyeza play kutazama…