Leo November 9 2016 Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametangaza kuvifutia usajili wa kudumu vyama vya Chama cha haki na ustawi ‘CHAUSTA’, African Progressive Party of Tanzania ‘APPT Maendeleo’ na Chama cha Jahazi Asilia.
Jaji Mutungi ameeleza hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwa zoezi hilo la uhakiki ilibainika kuwa, vyama vya siasa hivyo vitatu vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria ya vyama vya siasa, hivyo kila chama kilipewa taarifa ya nia ya msajili kufuta usajili wake wa kudumu na kutakiwa kujieleza kwa nini kisifutiwe.
Taarifa ya Jaji Mutungi imesema katika utetezi wao vyama hivyo vilishindwa kutoa sababu za kuridhisha kuwa havijakiuka sheria na bado vinazo sifa za usajili wa kudumu.
Mapungufu kwa ujumla wake ambayo yameonyeshwa kwenye kila taarifa ya kufuta usajili wa kudumu iliyopelekwa kwa chama husika ni haya……
- Kutokuwa na ofisi ya cham Tanzania Bara na Zanzibar kwa mujibu wa kifungu cha 10d
- Kutokuwa na uanachama Zanzibar kwa mujibu wa kifungu cha 10d.
- Kushindwa kuweka kumbukumbuza mapato na matumizi ya chama kwa mujibu wa kifungu cha 14(1)(a)
- Kushindwa kuwasilisha hesabu zake za mapato na matumizi ya mwaka kwa mtthibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili zikaguliwe kwa mujibu wa kifungu cha 14(1)(b)(i)
- Kushindwa kuwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa tamko la orodha ya mali za chama kwa mujibu wa kifungu cha 14(1)(b)(ii) au
- Kushindwa kutekeleza matakwa ya kifungu cha 15(1) kwamba mapato yote ya fedha ya chama yawekwe katika akaunti ya chama
Unaweza kutazama hii video hapa chini
VIDEO: Aliyoyazungumza Donald Trump punde tu baada ya kushinda Urais Marekani, ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
https://www.youtube.com/watch?v=oWY9t7Am3Jk