Ni zaidi ya mwezi mmoja umepita toka Charles Kitwanga kuvuliwa wadhifa wa Uwaziri wa mambo ya ndani ambapo Waziri huyu ambaye ni Mbunge wa Misungwi amezungumza na Waandishi wa habari nyumbani kwake na kuyasema yafuatayo.
- Baada ya yaliyotokea anaelekeza nguvu zake kuwatumikia na kuwaletea maendeleo Wananchi wa Misungwi ambapo kwenye hatua ya kwanza amekabidhi misaada mbalimbali yakiwemo magodoro 150 kwa idara ya afya.
- Yaliyopita sio ndwele, hilo ndio liwe jibu na Watanzania wote wasimuulize tena kuhusu kilichotokea.
- Anasema ‘Rais Magufuli kwanza nimpongeze sana, ni mtu namfahamu kidogo… ni Muadilifu, Msikivu na mimi siwezi kuhoji alichoamua, Rais anafanya vitu vingi mno vizuri tumuunge mkono, ni mtu mwema na anatenda aliyoyasema’
ULIYAKOSA MAMBO 9 KUHUSU RAY C BAADA YA KUCHUKULIWA NA POLISI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI