TatuMzuka, mchezo wa namba Tanzania leo November 6 2018 umewatambulisha washindi wawili wa milioni 80 walioshinda kupitia SupaMzuka jackpot iliyofanyika jumatano jijini Dar-es-salaam. Hii inakuwa mara ya tatu katika kipindi cha wiki wiki mbili kutoa kiasi kikubwa kwa washindi baada ya kutoa milioni 250 na milioni 60 mfululizo wiki iliyopita.
Hassan Abdallah Said ambaye ni machinga wa miwani visiwani Zanzibar na Baraka Jonas Chiute muuza nyama jijini Dar-es-salaam ndio walioibuka washindi kwa kubeba kitita cha milioni 40 kila mmoja huku wakichagua washkaji 10 wasiowajua kushiriki droo kubwa ya ‘Mamilionea 28 ndani ya usiku mmoja’ tarehe 28 Novemba 2018.
Akielezea furaha yake mmoja wa washindi Bwana Hassan Abdallah alisema hajawahi kuhisi kama siku moja angeweza kushinda kiasi kikubwa cha pesa na kuongeza kuwa hii ni fursa ya kubadili maisha yake.
“Nilipoona wengine wanashinda nikasema namimi bila shaka naweza kushinda. Kwa sasa ninayo furaha kubwa kwamba maisha yangu yamebadilika kwa sababu nitafungua duka langu mwenyewe na kujenga nyumba” aliongeza Abdallah
Mwanzoni mwa mwezi huu TatuMzuka ilitangaza nia yake ya kutengeneza washindi zaidi ili kutii kiu ya wachezaji wake kwa kuzindua kampeni ya ‘Mamilionea 100 ndani ya siku moja’ ambapo washindi 100 watapatikana usiku wa tarehe 28 Novemba.
“Tumeanza vizuri mwezi Novemba kwa kubadili maisha ya watanzania wawili lakini tumejipanga kutengeneza historia kwa kutengeneza washindi 100 ndani ya usiku moja. Katika jackpot iliyopita watanzania 10 wamejikatia tiketi ya kushiriki katika droo hiyo kubwa na tunaendelea kutoa hamasa kwa watanzania kuendelea kucheza ili kujikatia tiketi ya kushiriki katika jackpot hiyo ya kihistoria tarehe 28 Novemba mwaka huu” alihitimisha Bi. Patronila Mtatiro , Afisa uhusiano wa TatuMzuka
Ni furaha tu! Mshindi wa MILIONI 300 Tatu Mzuka alivyozipeleka kwao Mbagala, Unaweza kubonyeza play hapa chini kuitazama