Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Moja ya habari iliyoandikwa leo January 7 2017 ni pamoja na hii ya gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Gobore latumika sehemu ya mahari’
#NIPASHE Mila ya kutoa silaha aina ya Gobore kama sehemu ya mahari kwa kabila la Wapimbwe Katavi imetajwa kuchangia kuzagaa kwa silaha pic.twitter.com/4OVOBuVbmi
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
Gazeti hilo limeripoti kuwa mila ya kutoa silaha aina ya gobore kama sehemu ya mahari kwa kabila la Wapimbwe, waishio wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imetajwa kuwa moja ya sababu za kuongezeka kuzagaa kwa silaha mkoani hapo.
Mwanaume anapomuoa msichana katika kabila hilo, hutakiwa pamoja na mambo mengine kutoa gobore, hivyo kulazimika kutafuta watu wanaotengeneza magobore hayo ili wamtengenezee ili akalipe mahari na kupata mke.
Mmoja wa wazee wa kabila la Wapimbwe, Christopher Kapama, akizungumza na Gazeti la Nipashe alisema hiyo imekuwa ni sababu zinazochangia mkoa wa Katavi kuonekana kuna bunduki nyingi za aina ya magobore zikiwa zimezagaa maeneo mbalimbali.
Alisema kwa asili, kabila la Wapimbwe ni wawindaji na miaka ya nyuma walikuwa wanadai gobore kama sehemu ya mahari ili iwasaide katika shughuli zao, lakini kutokana na sheria za wanyamapori hivi sasa uwindaji wa aina hiyo ni haramu hivyo inabidi mila hiyo ibadilike.
Unaweza kuzipitia hapa chini habari zingine kubwa za magazeti ya leo January 7 2017
#NIPASHE Vigingi 9 kwa bosi TANESCO
1. Mikataba
2. Posho
3. Bei Mpya
4. Kukatika Umeme
5. Wizi
6. Urasimu
7. Rushwa
8. Manunuzi
9. Madeni pic.twitter.com/yUFctYBAP3
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#NIPASHE Rais Magufuli amelikumbuka jimbo lake la uchaguzi la Chato baada ya kutoa mil 10 kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya Muganza pic.twitter.com/QO4HB5j74g
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#NIPASHE Mila ya kutoa silaha aina ya Gobore kama sehemu ya mahari kwa kabila la Wapimbwe Katavi imetajwa kuchangia kuzagaa kwa silaha pic.twitter.com/4OVOBuVbmi
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#NIPASHE Wafanyabiashara wa pombe za kienyeji wilaya ya Siha K'njaro wamepigwa marufuku ya kutumia nafaka hasa mahindi kutengeneza vileo pic.twitter.com/k3O39xx9Na
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#NIPASHE Zaidi ya watoto 12,000 Dodoma wanaishi ktk mazingira hatarishi kutokana na kukosa matunzo kwenye familia zao pic.twitter.com/GZj6pg4dhz
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#JamboLEO Wasichana wa kazi watajwa chanzo cha kuvuruga ndoa DSM kutokana na uhusiano zaidi ya kazi za nyumbani wanaokuwa nao na mabosi wao pic.twitter.com/4zevT53v9k
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#JamboLEO Polisi Israel imefanya mahojiano ya saa tano na Waziri mkuu Netanyahu kwa mara ya pili kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili pic.twitter.com/7vmvV3kHBa
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#MWANANCHI TFDA imepiga marufuku uuzwaji wa vyakula, vipodozi na vifaatiba kwa njia ya mitandao ya kijamii pic.twitter.com/pBmSGm3Qtt
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#MWANANCHI Baraza la madiwani Mbeya limewafukuza kazi watumishi wanne kwa makosa tofauti likiwamo la udanganyifu na matumizi mabaya ya fedha pic.twitter.com/3THcWvpIWi
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#MWANANCHI Baadhi ya walimu Shinyanga wamegoma kuacha biashara za bodaboda nyakati wanazopaswa kufundisha licha ya kuonywa mara kadhaa pic.twitter.com/kCDYtCygjt
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#MWANANCHI Polisi Sengerema inawashikilia watu watano akiwamo mzee wa miaka 80 wanaodaiwa kukutwa wakilima ekari tatu za bangi pic.twitter.com/jmcmWPLcLC
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#HabariLEO Polisi kukamata magari yote ambayo yamewekwa taa zenye mwanga mkali kwa kuwa ni kinyume na sheria ya usalama barabarani pic.twitter.com/vAkkUIxb0F
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#HabariLEO Dk. Emmanuel Nchimbi amefuta kesi ya madai ya bil 1 aliyokuwa amemfungulia kada wa CCM, James Mwakibinga pic.twitter.com/lcF90hkOgn
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#HabariLEO Kati ya wanawake 350 na 450 hujifungua kila siku ktk hospitali za serikali jijini DSM na idadi hiyo haiendani na wauguzi waliopo pic.twitter.com/Dddtrs9Uvc
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#UHURU Upelelezi wa kesi ya kutakatisha fedha inayomkabili mfanyabiashara maarufu DSM, 'Pedeshee Ndama' haujakamilika pic.twitter.com/FxUcOY8728
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#UHURU SUMATRA Tanga kuendelea na operesheni ya kukagua na kuwachukulia hatua kali madereva wanaobainika kuzidisha abiria kwenye mabasi pic.twitter.com/uUvGWoyvXV
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#NIPASHE Serikali imeanza mazungumzo na taasisi za fedha nchini ili kukopa fedha kwa ajili ya kusaidia utekelezaji bajeti ya mwaka 2016/17 pic.twitter.com/EIT2ylz3f2
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#Tanzania DAIMA NHC kuanza kuvunja jengo la Bilicanas lililokuwa linamilikiwa na mfanyabiashara na mwanasiasa Freeman Mbowe pic.twitter.com/CgaMIm3lNa
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#MWANASPOTI Imeelezwa MO yuko karibu na uongozi Simba na anatoa mafungu kama alivyoahidi wakati alipoomba kuwekeza na hajakatishwa tamaa pic.twitter.com/3EAcpYDidd
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
#UHURU Kikosi cha usalama barabarani kimesema mbinu za kiintelijensia kuwanasa madereva wanaoendesha magari kwa mwendokasi ni zoezi endelevu pic.twitter.com/JKLDVM7zsV
— millardayo (@millardayo) January 7, 2017
AyoTVMAGAZETI: Vigingi 9 tishio kwa boss mpya TANESCO, Familia majeruhi 4,000 zaibebesha mzigo MOI