Staa wa kimataifa wa Brazil anayecheza soka la kulipwa katika club ya Juventus ya Italia Douglas Costa amepata ajali ya gari lake binafsi akiwa katika mizunguuko yake binafsi, Costa inaripotiwa alikuwa njiani anarejea katika mji wa Turin.
Imeripotiwa kuwa Polisi bado wanachunguza chanzo cha ajali hiyo ambayo bado haijajulikana iliyohusisha gari la Costa, inaelezwa kuwa Costa ambaye amefanikiwa kutoka salama na gari lake pekee ndio kuumia alikuwa katika matembezi yake binafsi baada ya timu yao kupewa mapumziko ya siku mbili baada ya game dhidi ya Parma iliyomalizika kwa sare ya 3-3.
Douglas Costa alikuwa anaendesha gari yake aina ya Jeep Chorekee na dereva wa gari aina ya Fiat Pinto amepelekwa hospital kwa ajili ya kuangaliwa vizuri, hiyo ni baada ya kuumia katika ajali hiyo, Douglas Costa imeelezwa kuwa yupo sawa.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF