Shirika la umeme Tanzania ‘TANESCO’ kupitia kwa Kaimu mkurugenzi mtendaji, Dr. Tito Mwinuka leo march 9 2017 amekutana na waandishi wa habari na kusema kuwa shirika hilo linakusudia kuendesha zoezi la ukusanyaji wa madeni ya bill za umeme zilizolimbikizwa na wateja mbalimbali nchi nzima.
Dr. Tito Mwinuka amesema madeni hayo yanajumuisha madeni ya wateja wadogo, wizara, taasisi mbalimbali za serikali pamoja na makampuni binafsi na amesema wadaiwa wote watatakiwa kulipa madeni yao ndani ya kipindi cha siku 14, baada ya hapo itasitisha huduma kwa wateja watakaoshindwa kuanza kulipa madeni yao na hatua zingine za kisheria.
Unaweza kubonyeza play hapa chini kutazama
VIDEO: Mbowe aliposhiriki msiba wa mama yake mdogo Rais Mstaafu Kikwete, Bonyeza play hapa chini kutazama