Chama cha wahasibu Tanzania (TAA) kwa kushirikiana na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) pamoja na chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) kimetoa taarifa rasmi kuanza kwa “Wiki ya Uhasibu”
Kwa mwaka 2020 Wiki ya Uhasibu itaadhimishwa kwa siku 6 kuanzia March 9 hadi March 14, Wiki ya Uhasibu inafanyika kwa ajili ya kuifahamisha jamii umuhimu wa taalum ya uhasibu kwa ajili ya uchumi wa viwanda na maendeleo ya jamii.
Hii itakuwa inawaleta pamoja wadau mbalimbali kushiriki na kutambua kazi ya Uhasibu na Wahasibu wanaofanya kazi katika taasisi mbalimbali kwenye ngazi mbalimbali za majukumu ya taaluma hiyo, ambapo kutakuwa na huduma ya kushauri na kuwawezesha wahasibu kusonga mbele kitaaluma.
Kwa Wahasibu ambao wana malengo ya kufungua kampuni zao binafsi au taasisi zozote za Uhasibu hiyo itakuwa ni fursa nzuri kwao kukutana na wenye makampuni wabobemzi na itakuwa ni fursa nzuri kushea nao mawazo.
VIDEO: PAMBANO LA ROUND 10: MTANZANIA VS MTHAILAND NI UBINGWA WA DUNIA