Mkuu wa Wilaya ya Kisare Jokate Mwegelo ameeleza maamuzi yaliyofikiwa na uwongozi wa Wilaya ya Kisarawe kufuatia changamoto ya upungufu wa Sukari uliojitokeza Kisarawe.
Jokate ameeleza kuwa leo May 4,2020 kimefanyika kikao na kufikia muafaka wa upatikanaji wa sukari wilyani humo tena kwa bei elekezi waliyokubaliana na wafanyabiashara.
….>>>”Kutokana na changamoto iliyojitokeza ya ukosefu wa sukari Wilaya ya Kisarawe, Uongozi wa Wilaya (DED, DAS), Afisa Biashara wakishirikiana na wawakilishi wa wafanyabiashara wa Kisarawe Leo tarehe 4/05/2020 kimefanyika kikao kufikia muafaka wa upatikanaji wa sukari kwa Bei Elekezi kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali kwa kupitia GN 284 ya tarehe 24/04/2020 iliyotoa Bei elekezi za ukomo kwa wauzaji wa sukari wa jumla na rejareja kwa Mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
”Wafanyabiashara wamekubali kuhakikisha sukari inapatikana kuanzia leo 4/05/2020 kwa Bei elekezi kwa maeneo yote ya Wilaya ya Kisarawe. Bei elekezi za ukomo kwa Mkoa Pwani ni 2,250/= kwa wauzaji wa jumla na 2,700/= kwa wauzaji wa rejareja hivyo Wananchi wa Kisarawe watapata sukari kwa bei isiyozidi bei ya ukomo 2,700/= na sukari itapatikana kuanzia leo.”
“Ofisi ya Mkuu Wa Wilaya Ya Kisarawe Inatoa Pole Kwa Wananchi Wote wa Kisarawe Kwa Changamoto Zote Zilizojitokeza.”
Bonyeza PLAY hapa chini kusikia zaidi