Top Stories

Kutokea Ubalozi wa Kenya ‘Corona isitugombanishe,tutalimaliza’

on

NI Mei 19, 2020 ambapo Ubalozi wa Kenya kupitia la balozi wake aitwae Kazungu amefanya mkutano wa waandishi wa habari kwa kile kinachoendelea mitandaoni.

“Rais Kenyatta amenituma hapa, anasema Kenya haiiangalii Tanzania kama jirani bali kama Ndugu, sisi sio maadui, adui yetu ni corona, ndio maana alikuwa Rais wa kwanza kuingia Chato kumsalimia JPM, akachukua dhahabu akasema mpelekeeni Maguful -Dany Kazungu, Balozi wa Kenya nchini Tanzania

Bila hii Corona April 26 mwaka huu Kenyatta alipanga aje asherehekee na Watanzania Muungano, alipanga awe na ziara ya muda mrefu hapa TZ kuliko Rais yeyote, uamuzi ambao Kenya imechukua kuhusu safari za mipakani sio kwasababu ya Tanzania bali adui yetu ni kirusi”-Balozi Kazungu

Hakuna Mkenya anayemuombea mabaya Mtanzania, Wakenya tunawaombea Watanzania mpigane na janga hili, na sisi pia mtuombee, tusianze kukorogwa na kirusi hiki, tusianze kugongana kisa corona, Watu watulie, Viongozi wetu watakutana na tutalimaliza” -Balozi Kazungu

Soma na hizi

Tupia Comments