Uvutaji wa tumbaku zenye ladha tofautitofauti ambazo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija (Shisha) umeshika kasi kwa sasa huku baadhi ya Watumiaji wakihisi huenda Shisha haina madhara lakini Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema matumizi ya Shisha ni hatari zaidi kwa afya .
Kamishina Msaidizi Kitengo cha Kinga na Huduma za Jamii wa DCEA, Moza Makumbuli akiwa Morogoro leo amesema kwa mujibu wa tafiti Mtu anapovuta Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta wastani wa sigara 100 hadi 200.
Moza amesema kifaa cha Shisha ni kwa ajili ya matumizi ya tumbaku lakini baadhi ya Watumiaji hutumia kifaa hicho kuchanganyia dawa za kulevya kitendo ambacho ni hatari zaidi.