Wekundu wa Msimbazi Simba leo Jumapili ya October 15 2017 walikuwa uwanja wa Uhuru kuwakaribisha Mtibwa Sugar kwenye game yao ya sita ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018.
Wamekutana leo kwa mara ya 7 toka mwaka 2014 ambapo kati ya mara zote saba, Mtibwa haijawahi kumfunga Simba ambapo imekubali vipigo mara nne na kutoa sare 3 ikiwemo game ya leo iliyomalizika kwa sare ya 1-1.
Leo October 15 2017 ilikua bado kidogo Mtibwa Sugar waingie katika historia mpya ya kuifunga Simba kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitatu katika Ligi Kuu kwani hadi dakika ya 90 Mtibwa Sugar walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0 lililokuwa limefungwa na Stamili Mbonde dakika ya 36.
Upepo ulibadilika baada ya makosa kufanywa na mabeki wa Mtibwa Sugar dakika za nyongeza kipindi cha pili kwa kumchezea faulo Erasto Nyoni sentimita chache kutoka eneo la hatari ambapo Emmanuel Okwi alipiga faulo iliyotinga wavuni moja kwa moja.
Sare ya leo inaifanya Simba kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli ya kushinda na kufunga kwani ina point 12 sawa na Yanga, Mtibwa na Azam FC, hizi hapa chini ni baadhi ya picha kutoka kwenye game ya leo
ULIPITWA? List ya majina 30 ya wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017
MAGOLI YOTE: Taifa Stars vs Malawi FT 1-1…. yatazame kwenye hii video hapa chini
UNATAKA KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI? Breaking NEWS, Za Mastaa, Siasa, Michezo na nyingine…. fanya jambo moja tu rahisi… BONYEZA PAGE ZIFUATAZO ili nikutumie kila kitu kiganjani mwako >>> INSTAGRAM <<<< FACEBOOK >>>> TWITTER <<<< na ili kupata BREAKING NEWS zote kwa njia ya video ingia HAPA kisha bonyeza SUBSCRIBE