Leo November 9 2016 Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametangaza kuvifutia usajili wa kudumu vyama vya Chama cha haki na ustawi ‘CHAUSTA’, African Progressive Party of Tanzania ‘APPT Maendeleo’ na Chama cha Jahazi Asilia.
Taarifa aliyoitoa Jaji Mutungi imesema kwamba Mchakato wa kufuta usajili wa kudumu wa vyama hivyo unatokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya kisheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu uliofanyika kuanzia June 26 mpaka July 26 2016.
Jaji Mutungi ameeleza kuwa zoezi hilo la uhakiki ilibainika kuwa, vyama vya siasa hivyo vitatu vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria ya vyama vya siasa, hivyo kila chama kilipewa taarifa ya nia ya msajili kufuta usajili wake wa kudumu na kutakiwa kujieleza kwa nini kisifutiwe.
Taarifa ya Jaji Mutungi imesema katika utetezi wao vyama hivyo vilishindwa kutoa sababu za kuridhisha kuwa havijakiuka sheria na bado vinazo sifa za usajili wa kudumu.
Msajili wa vyama vya siasa nchini amevifutia usajili wa kudumu vyama vya CHAUSTA, APPT Maendeleo na Jahazi Asilia baada ya zoezi la uhakiki pic.twitter.com/soaQSgk66t
— millardayo (@millardayo) November 9, 2016
VIDEO: Maoni ya Zitto Kabwe kuhusu mkataba wa EPA ‘Tujiulize mara mbilimbili kwanini Kenya wamesaini?‘ TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI