Duniani

Watu na akili zao… walimtuma huyu Njiwa apeleke simu Gerezani

on

Brazil inatajwa kuwa nchi ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya Wafungwa gerezani ambapo ina Wafungwa 600,000 kwenye magereza yake na kama unakumbuka hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kihalifu ndani ya Magereza na yamesababisha vifo vya wafungwa 140.

Sasa kingine kilichoripotiwa ni kutokea kwenye gereza la Franco da Rocha ambapo Njiwa amekamatwa na Askari akipeleka simu ya mkononi kwa mfungwa ambapo bado haijafahamika aliyekuwa akimtumia Ndege huyo kupeleka simu.

Kuna maswali mengi ya kujiuliza lakini hayajajibiwa…. Njiwa huyo alielekezwa vipi? akili gani imetumika kumuongoza? alikua anatumia njia gani kuikabidhi simu?

Mfungwa Mtanzania gerezani China alivyompigia simu Millard Ayo, Bonyeza play hapa chini kusikiliza

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako Millard Ayo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments