Top Stories

Lema kafika Mahakamani tena leo…fahamu kilichoendelea (+VideoFUPI)

on

Kesi ya kuhamasisha wananchi kufanya maandamano ya UKUTA ambayo inamkabili Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema imeahirishwa hadi September 27, 2017 kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya hukumu.

Wakili wa Lema Sheck Mfinanga amesema kuwa upande wa Jamhuri ulitokea Mahakamani lakini pamoja na yote ulidai haukupatiwa nakala kwa ajili ya kuja kwenye rufaa na baada ya kupitia ikaonekana kuwa tarehe za nyuma aliwahi kuwa Wakili wa Serikali mwingine.

Aidha amesema kuwa upande wa Jamhuri uliomba kujibizana kwa njia ya maandishi ambapo Mahakama iliridhia na kupanga September 27, 2017 kwa ajili ya uamuzi.

ULIPITWA? Walichosema Lema na Mnyika kuhusu mauaji ya Kibiti…tazama kwenye video hii!!

Soma na hizi

Tupia Comments