Ripoti iliyotoka mwaka 2014 inayohusu idadi ya watu duniani ilionyesha China ina watu bilioni 1.3..Katika vitu ambavyo walivifanya ili kupunguza watu walipitisha sheria ya kila wanandoa mwisho wa kuzaa ni mtoto mmoja.
Kuna hii nyingine imetokea nchini humo ambapo kampuni moja imepanga kutoa masharti kwa wafanyikazi wake watakiwa kupata ruhusa kabla ya kupata watoto.
Wanawake wote walio kwenye ndoa wanaofikiria kupata watoto lazima wawe wamefanya kazi kwa mwaka mmoja kwenye kampuni hiyo kabla ya kutuma kibali cha kukubaliwa kushika mimba.
Kama ikitokea umekiuka sheria hiyo atakayeshika mimba atatozwa faini na pia kushushwa cheo kama alikuwa nacho.
Shirika la utangazaji la China limekosoa vikali kampuni hiyo na kusema haina ubinadamu kwa wafanyikazi wake.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.