Hii imetokea jana huko katika vijiji vya Kaskazini mwa India baada ya chui kuvamia..katika pitapita alikutana na maji yaliyokuwa ndani ya chungu na kuanza kunywa lakini alishindwa kutoka ndani ya chungu hicho na kujikuta akiondoka nacho.
Taarifa hiyo iliripotiwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo na kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ambapo katika video alionekana chuo huyo akijitahidi kujitoa lakini haikuwezekana hadi walipokuja maafisa wa wanyama pori.
Iliwachukua zaidi ya masaa sita kwa maofisa hao kuweza kufanikisha zoezi hilo la kumtoa kisha kumrejesha kwenye hifadhi yake.