Mei 30 2016 Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge iliwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano wa nne.
Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.
Leo May 31 2016 Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt. Helen kijo-Bisimba amekutana na waandishi wa habari na kutoa tamko lao kwa kinachoendelea bungeni……….
“Wabunge wote waliosimamishwa kuhudhuria vikao warudishwe bungeni kwani kufanya hivyo ni kuwakosesha wananchi haki yao uwakilishi kwani wabunge hao wamesimamishwa wakiwatetea wananchi wao“
Kituo cha sheria na haki za binadamu kimeguswa pia kuhusu wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma waliorudishwa majumbani kwao……….>>>Tunaitaka serikali isitishe uamuzi wake wa kuwafukuza wanafunzi wote wa UDOM na badala yake itafute suluhu kwa njia ya amani na iwadhibu wale wote waliohusika na sakata hilo:- Dkt. Helen kijo-Bisimba
ULIIKOSA HII YA FREEMAN MBOWE ALICHOZUNGUMZA BAADA YA UPINZANI KUTOLEWA TENA BUNGENI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE