Michezo

Tayari ninazo video za magoli ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mtu wangu…

on

September 29 michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, miongoni mwa mechi zilizovuta hisia za watu wengi ni mechi ya Arsenal dhidi ya Olympiakos, mechi ambayo ilimalizika kwa klabu ya Arsenal kupoteza mechi hiyo katika uwanja wake wa nyumbani kwa jumla ya goli  2-3.

Video ya magoli ya Arsenal 2-3 Olympiakos

https://youtu.be/01L6ouEFZ8I

Mchezo mwingine uliokuwa ukivutia ni mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Bayer Leverkusen mechi ambayo ilimalizika kwa klabu ya FC Barcelona kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-1 mechi iliyochezwa katika uwanja wa Camp Nou.

Video ya magoli ya FC Barcelona 2-1 Bayer Leverkusen

https://youtu.be/Sq4JFuHtlYU

FC Bayern Munich walikuwa wenyeji wa Dinamo Zagreb katika uwanja wa Allianz Arena, mchezo ambao ulimalizika kwa FC Bayern Munich kuibuka na ushindi wa idadi kubwa ya magoli kwani ilishinda jumla ya goli 5-0.

Video ya magoli FC Bayern Munich 5-0 Dinamo Zagreb

https://youtu.be/7Ratk9qcuBw

Klabu ya Chelsea chini ya kocha wake Jose Mourinho walisafiri hadi Ureno kuifuata FC Porto katika uwanja wa Estadio do Dragao, mahali ambapo Jose Mourinho ana historia na heshima kubwa katika uwanja huo ila kwa bahati mbaya Chelsea walipoteza mchezo huo kwa jumla ya goli 2-1.

Video ya magoli FC Porto 2-1 Chelsea

https://youtu.be/6hRUudB2EQ8

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments