Nchini Ujerumani wametengeneza Ndege aina ya LILIUM kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yenye siti mbili, shepu ya yai na inatumia umeme, imetengenezwa na mainjinia wanne wakijerumani wakidai kuwa ndege hiyo yenye kupunguza matumizi na kurahisisha usafiri kwa watu.
Ndege hii inasemekana kuwa na uwezo wa kwenda hadi spidi ya kilometa 400 kwa saa, kutumika kwenye eneo tambarare, kupaa na kutua kwa mita 15. Kingine kikubwa ni kwamba inatumia umeme na inachajiwa kama simu pia haina kelele pia ni kwa ajili matumizi ya mchana tu kwenye hali ya hewa tulivu na sio usiku.
Mmoja wa msaidizi wa mmiliki wa ndege hiyo, Daniel weigand amesema wana mpango wa kuiingiza sokoni mwaka 2018, ameyazungumza haya …………
>>>”tunataka ndege isiyo na gharama kubwa wala isiyokuwa na tatizo la utumiaji wa miundombinu yake, pia iweze kutumika na watu wengi wenye uwezo wowote ule sio watu wenye uwezo mkubwa tu ndo waweze kununua ndege hii”.
ULIKOSA MUONEKANO HUU WA BARABARA ZA K/KOO BAADA YA WAMACHINGA KUONDOLEWA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE