Rais Magufuli alitoa amri ya kuzuia kuagiza sukari toka nje ya nchi akieleza kwamba viwanda vya sukari wana sukari hiyo na wanashindwa kuuza kwa sababu ya sukari iliyoagizwa kutoka nje. Baada ya tamko hilo Serikali ilitangaza bei elekezi ya shilingi 1800 kwa kilo nchi nzima.
Leo May 13 2016 aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia sakata la sukari
Prof. Lipumba amemshauri Rais Magufuli kuruhusu uingizaji wa sukari kutoka nje kwa sababu viwanda vyetu vya ndani vya sukari havitoshelezi mahitaji ya sukari kwa wananchi na pia amesema vimesimama kuzalisha sukari kwa zaidi miezi sasa.
Prof. Lipumba amesema …….>>>’Takukuru badala ya kuwakamata Tegeta Escrow Account wanashughulikia sasa wanaoficha sukari, takwimu za wizara ya kilimo zinaeleza, nchini hakuna sukari ya kutosha lakini watu wanashughulika na kuitafuta sukari’
>>>‘pamoja na msako mkali sukari iliyokamatwa nchi nzima haifiki tani 10000 lakini kwa kuwa Rais ameshasema sukari imefichwa viongozi nao wanarudia kauli hiyo kuwa sukari imefichwa yasije yakawakuta yaliyomsibu mama Anne Kilango Malecela‘
ULIIKOSA HII YA PAUL MAKONDA MGUU KWA MGUU KWENYE MSAKO WA SUKARI DSM MAY 11? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE