Leo September, 15, 2020 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema atatahakikisha Bajeti ya Wizara ya Afya inapanda na kufikia asilimia 15 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Akihutubia Wananchi amesema, ongezeko la bajeti litawezesha katika kuandaa miundombinu ya Kisasa, Wataalam, Vifaa Tiba na Vipimo vya kutosha kwa maradhi yote.
Aidha, ongezeko la bajeti litawezesha kutenga fungu maalum kwa ajili ya kukabili maradhi ya milipuko kama COVID-19 kwa kadiri yatakavyojitokeza.
“Serikali ya Umoja wa Kitaifa itahakikisha 70% ya Watanzania wana Bima ya Afya ifikapo 2025 na 100% ifikapo 2028, hatua maalumu zitachukuliwa kuhakikisha huduma za uzazi bila malipo zinapatikana kwa kila Mama Mjamzito ili kupunguza vifo vingi vinavyotokea ambavyo vinadhibitika” Lipumba