Kumekuwa na tarifa ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni zikieleza kuwa Rais wa chama cha mawakili Tanganyika ‘TLS’, Tundu Lissu amealikwa kwenye mkutano mkubwa wa wanasheria duniani na atahutubia mkutano huo Marekani, taarifa hizo zilieleza kuwa Lissu atakuwa ni mwanasheria pekee kutoka bara la Afrika aliyepata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.
Sasa AyoTV imempata Tundu Lissu na kumuuliza ni kweli amealikwa kuhutubia mkutano wa wanasheria duniani. Akijibu swali hilo Lissu amesema taarifa hizo si za kweli na yeye ameona tu kwenye mitandao. Unaweza kubonyeza play hapa chini kuitazama hii video hii hapa chini
LISSU MAHAKAMANI TENA: Ni kwenye kesi ya ‘Dikteta Uchwara’ inayomkabili, Bonyeza play hapa chini kutazama