Kesi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake watatu ambao wanatuhumiwa kwa kufanya uchochezi kupitia gazeti la mawio kwenye habari yenye kichwa kinachosema ‘Zanzibar Machafuko yaja‘ imeendelea leo June 28 2016 kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.
Mahakama hiyo imeyaondoa mashtaka mawili ya uchochezi kati ya matano katika kesi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake watatu.
Mbali ya Lissu ambaye alisomewa mashtaka yake leo kutokana na awali kutofika mahakamani hapo wakati wenzake wakisomewa, wengine katika kesi hiyo ni mwandishi wa gazeti la Mawio, Jabir Idrissa, mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina na mchapishaji wa kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.
Akimsomea mashtaka hayo, wakili Kadushi alidai kuwa Lissu anakabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa za uchochezi na shtaka la pili linalomkabili pamoja na wenzake kuwa January 14 2016 jiji la Dar es Salaam, wanadaiwa kuchapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.
Aidha inadaiwa mnamo January 14 2016, jijini Dar es Salaam, Lissu na wenzake bila ya kuwa na mamlaka yoyote yale, waliwatishia na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar ili wasiweze kuingia kwenye marudio ya uchaguzi mkuu.
Baada ya kumsomea mashtaka hayo Lissu aliyepandishwa kizimbani alikana kutenda makosa hayo. Kutokana na mvutano kisheria ulioibuka mahakamani hapo kutoka pande zote mbili,Hakimu Simba alisema uamuzi wa kufutwa ama kutofutwa utatolewa July 11 2016 pia Lissu ameachiwa kwa dhamana.
ULIKOSA HII YA TUNDU LISSU KUWASILISHA MAONI HAYA KUHUSU SERIKALI YA MAGUFULI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE