Mchezaji kutoka Afrika ili aweze kucheza Ligi Kuu Uingereza moja kwa moja mara nyingi hadi taifa lake liwe katika viwango vya juu vya FIFA, vinginevyo lazima apite Ligi nyingine barani Ulaya ndio apate nafasi ya kucheza Uingereza.
March 19 mtu wangu wa nguvu kutoka sokka.com nimekutana na list ya rekodi ya wachezaji watano wa kiafrika waliopata bahati ya kucheza Ligi Kuu Uingereza na kuweka rekodi ya kuwa katika TOP 5 ya wachezaji wa Afrika wanaoongoza kwa ufungaji kwa muda wote EPL.
5- Nwankwo Kanu– magoli 54 (Nigeria), Kanu amewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal,West Brom and Portsmouth. Kanu pia amewahi kushinda mataji ya mchezaji bora wa Afrika mara mbili, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja na mataji matatu ya FA.
4-Yaya Toure – magoli 55 (Ivory Coast). Baada ya kuondoka FC Barcelona mwaka 2010 na kujiunga na Man City ya Uingereza, staa huyo nyota yake imezidi kung’aa, kwani kwa kiungo kuwa na idadi hiyo ya magoli inatajwa kuwa sio mbaya.
3- Yakubu Aiyegbeni– magoli 96 (Nigeria). Nyota yake iling’aa msimu wa 2002/2003 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu ya Maccabi Haifa ndio alipopata nafasi ya kuanza kucheza Uingereza kwa mkopo akiwa na klabu ya Portsmouth na baadae vilabu vya Middlesbrough, Everton na Blackburn Rovers.
2- Emmanuel Adebayor – magoli 97 (Togo). Sheyi Emmanuel Adebayor ambaye alizaliwa 26 February 1984 Lome,Togo kutoka kwa wazazi wenye asili ya Nigeria, amempiku Yakubu baada ya kufunga goli lake la kwanza akiwa na Crystal Palace hivi karibuni. Adebayor amewahi kucheza vilabu vya Uingereza kama Arsenal, Manchester City na Tottenham.
1- Didier Drogba– magoli 104 (Ivory Coast). Drogba amefanikiwa kufunga magoli 104 na kuwa mwafrika anayeoongoza kwa magoli mengi Ligi Kuu Uingereza akiwa ameichezea klabu moja tu Uingereza Chelsea. Adebayor bado anayo nafasi ya kumpiku Drogba kwani bado anacheza Uingereza.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE