Mix

Maneno ya Polisi Dar baada ya kuwasili kwa Tundu Lissu leo

on

Agosti 3, 2016 kulikuwa na taarifa za kukamatwa kwa mwanasheria ambae ni mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu akiwa kwenye mkutano wake katika kijijini Ikungi Singida.
Sasa basi mwanasheria huyo ameshawasili leo jioni Agosti 4, 216 Dar es Salaam kwaajili ya mahojiano na Polisi kutokana na maneno aliyoyazungumza Agosti 2,2016 kusadikiwa kuwa ni ya uchochezi kwa Serikali pamoja viongozi wa nchini.
UCHWAA
Millardayo.com & Ayo TV imempata Naibu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya kayaongea haya>>Tumeshampata yupo na tunaendelea kumhoji kuhusiana na kauli zake alizozitoa siku ya Agosti 2, 2016 pale Mahakamani, amefika majira ya jioni Dar es Salaam kwahiyo tunaendelea na mahojiano kwani alitoa kashfa kwa Serikali alitoa Kashfa kwa Kiongozi’- Polisi

Sasa yeye ni Mwanasheria lakini anatoa maneno ya uchochezi kwahiyo kama Jeshi la polisi lazima tumshurutishe ili awe makini na sheria za nchini na mwisho wa siku baada ya mahojiano tutampeleka Mahakamani’– Polisi

ULIIKOSA HII KAULI YA TUNDU LISSU BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI AGOSTI 2, 2016 BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments