Ni Agosti 25, 2021 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amehudhuria ufunguzi wa kikao cha maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na makamanda wa Polisi wa mikoa/vikosi Dar es Salaam.
“Changamoto zingine zinahusu ucheleweshwaji wa upelelezi pamoja na kukosekana ama kupungua kwa uadilifu,nidhamu na maadili kwa baadhi ya maskari wetu, kesi nyingi zinakwama Mahakamani kutokana na kucheleweshwa kwa upelelezi au kwamba hazina ushahidi na hizi ndio zile tunaziita kesi za kubambikizwa”- Rais Samia
“Lakini nina wapongeza kwa uamuzi wenu kwa kuweka ukomo wa kufanya upelelezi kufikia miezi sita kwa zile kesi ndogo ndogo lakini mwaka mmoja kwa zile kesi kubwa lakini bado tunaweza kufanya vizuri zaidi”- Rais Samia
“Kwasababu kucheleweshwa kwa upelelezi kunaongeza mzigo mkubwa kwa Serikali kuweka Mahabusu Jela, tukiangalia takwimu mpaka mwezi huu tarehe 22 idadi ya Mahabusu katika jela zetu karibu sawa sawa na idadi ya wafungwa katika Jela zetu”-Rais Samia
“Wafungwa walikuwa 16,542 lakini Mahabusu ni 15,194 mpaka juzi, sasa Mahabusu hawa kuna walikaa wiki, miaka mitatu, mwaka, muda mbalimbali na kila anaeguswa upelelezi haujakamilika sasa nitoe wito mara mbili”-Rais samia
“Kwa zile kesi ambazo mna hakika upelelezi hautokamilika hao watu watolewe, wakafaidi huru wao wakiwa nje kama kesi haina mwelekeo basi hao watu watolewe lakini zile kesi ambazo mna uhakika upelelezi utatimia basi ziharakishwe”- Rais Samia
“Kwa upande mwingine Mwanadamu ni Mwanadamu na ana uhuru wake naomba mkae na wadau wengine muangalie uwezekano wa kurekebisha sheria ya kumuweka mtu mahabusu”- Rais Samia
“Tuko hapa kuhudumia watu na si kudidimiza watu, ni aibu kuona kwenye simu zetu tunarushiwa clip Askari wa Jeshi la Polisi anakubaliana na raia achukue rushwa”- Rais Samia
“Hasa Jeshi la Traffic huko upande wa Traffic na hawajui kwamba maendeleo ya Teknolojia haya, mtu aliekuwemo ndani ya gari anamrekodi kwa kalamu tu na wala sio hata simu, kwahiyo naomba mkayaangalie hayo muende mkayashughulikie tuondoe hiyo aibu”- Rais Samia
Ayo TV iko mubashara muda huu unaweza ukabonyeza play kufuatilia live hafla hiyo