NI July 30, 2021 ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Mohammed Dewji anazungumza na wanahabari .
“Mimi si mnasema ni mwekezaji simba bajeti ndogo hatuna Pesa kwa hivyo waandishi wa habari mimi kwenye miaka minne nimewekeza yaani hapa mpaka leo Bilioni 21. 3 na kila pesa ambayo nimetoa utaniuliza hizi Pesa umetoa kwenye nini kila mwezi tunasajili wachezaji kwahiyo nilikuwa nataka mafanikio kwenye timu’-Mo Dewji
“kwahiyo mimi kila mwaka nilikuwa natoka zaidi ya Bilioni 5 kwa miaka minne hapo Bilioni 21.3 tunaingia kwenye Pre Season lazima nilipe mimi, tunaenda kununua wachezaji lazima nilipe mimi hizi ni Pesa za ziada kwasababu naipenda Simba”- Mo Dewji
“Lakini Kitu kinachoniumiza mimi sana maneno yanayosemwa kwamba mimi sina Bilioni 20 sasa leo hii nimetumia Bilioni 21.3 kwa hesabu zangu za haraka haraka itafika bilioni 24 tayari lakini leo hii nikisimama mbele yenu nikisema nimetimza hiyo Bilioni 24”- Mo Dewji
“Si hakuna anaenidai kwahiyo hisa zangu za 49% ni Bilioni 19.9 mwishoni tulianza Bilioni 20 nipate 51% halafu mmefika Bilioni 20 nipate 50% halafu Bilioni 20 imekua 49% kwahiyo Bilioni 19.6 kelele itaanza wachambuzi watasema Bilioni 20 mbona kabadili”- Mo Dewji
“Leo hii natoa rasmi Bilioni 20 hapa mbele ya waandishi wa habari huu mzozo uishi kila kitu namaliza hapa mbele ya waandishi wa habari lakini mjue sasa sinunui hisa ya 49% kwa 19.6 lakini naweza kufika Bilioni 13 ama Bilioni 14 maana yake thamani ya Club imeshuka lakini imezidi kutokana na uwekezaji”- Mo Dewji
“Natukubaliane kwamba Simba imeweka ligi yetu ya Tanzania kwenye ramani ya Afrika mimi nasafiri sana kila nikisafiri nasikia sana Simba kwahivyo niwapongeza bodi Mwenyekiti wathamini kwa kufanikisha kuweza kuwaongoza vizuri”- Mo Dewji
“Mjue kwamba nina mapenzi na Simba sisi tulifungwa na Prison nililia sana Pesa sio muhimu lakini Muda ndio muhimu sana kwahiyo mjue mimi kitu kimoja naipenda sana Simba kwa dhati nawekezaji kwenye Simba sio kupata pesa unajua leo ligi yetu imekuwa kubwa kuwa watu wanapata wadhamini kutokana na mgongo wa Simba lakini wafanyabiashara wanapata Pesa mimi sifanyi hivyo “- Mo Dewji
“Nakuambia kwenye miaka ishirini ijayo Simba haitoweza kuzalisha Pesa”- Mo Dewji