Muimbaji Yvonne Sangudi mkazi wa California Marekani mwenye asili ya Tanzania amekutana na mtayarishaji na rapper mkongwe kwenye game ya Hip Hop Marekani Jazze Pha usiku wa August 30,2018 kwenye ugawaji wa tuzo za RnB na Hip Hop.
Katika maongezi waliyoyafanya Jazze Pha ameahidi kuitembelea Tanzania hivi karibuni, rappa huyo aliwahi kufanya kazi na mastaa wakali wakiwemo Ciara, T.I, Ludacris,Snoop Dogg, pia amechukua umaarufu mkubwa ikiwemo kutengeneza baadhi ya ngoma za legends kama 2Pac.
Yvonne Sangudi ametudokeza pia kuhusiana na ujio wa ngoma yake mpya aliyoifanya na A.Y wakiwa pamoja California, Marekani. Yvonne Sangudi alitambulika na ngoma ya Tanzanite miaka minne iliyopita.
“Rich Mavoko hana stress, hajapungua mwili anafanya mazoezi, siwezi mkana” Lulu Diva