Baada ya kusimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema moyo wake una amani kwani mahusiano yake na haki yanazidi kuimarika.
Lema ameandika ujumbe huo muda mfupi baada ya Bunge kutoa maamuzi ikiwa ni siku moja baada ya Kamati ya Maadili kumhoji kwa kuunga mkono kauli ya CAG kwamba Bunge ni dhaifu.
“Nimesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge mpaka January 2020. Moyo wangu una amani sana, kwani mahusiano yangu na haki yanaendelea kuimarika zaidi. Nawatakia Wabunge wenzangu kazi njema katika wajibu huu, sitanyamaza hata kama adhabu itakuwa ni mauti” Lema
DC, MTOTO WA MAMA NTILIE NDELE MWASELELA, WAPIGA DEBE BEGA KWA BEGA NA MAGUFULI MBEYA