Mtu wangu wa nguvu najua unafahamu kama mchezo wa soka ndio mchezo unaoongoza kwa kupendwa duniani. Katika soka kuna list ya wachezaji ambao wanapendwa na mashabiki kutokana na vitu ambavyo wanafanya uwanjani. Imenifikia TOP 5 ya mastaa wa soka wanaoongoza kwa kupendwa duniani stori kutoka givemesport.com
Lionel Messi ambaye anaichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania ndio anatufungulia list hii, Messi amekuwa kivutio kikubwa pindi anapotembelea nchi tofauti tofauti. Messi alipata usumbufu mkubwa, wakati alipo safiri kuelekea Japan kucheza michuano ya Kombe la klabu bingwa Dunia mwaka 2011 dhidi ya Santos.
Thierry Henry ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, anakumbukwa kwa mchango wake aliouonyesha wakati anaichezea klabu ya Arsenal kitu ambacho kilimfanya apendwe na mashabiki wa soka, Henry ana asili ya upole suala ambalo limemuongezea upendo kwa mashabiki.
Xavi Hernandez hakuna shabiki wa FC Barcelona asiyemfahamu huyu jamaa, ni kiungo wa kati ambaye alikuwa kiongozi kwa wachezaji wenzake wa FC Barcelona, kitendo cha kukaa kwa muda mrefu na timu hiyo kimemfanya apendwe zaidi na mashabiki wa soka. Xavi amekuwa mtu muhimu kwenye kutatua matatizo . Sasa hivi anaichezea klabu ya Al Sadd SC iliyopo Qatar.
Paul Scholes ni moja kati ya wachezaji bora wa muda wote katika kikosi cha Manchester United kuwahi kutokea katika nafasi ya kiungo, anakumbukwa kwa goli alilofunga dhidi ya FC Barcelona na kuwatoa katika michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu wa 2008/2009.
David Beckham ni jina ambalo watu wengi wamelizoea, amewahi kuvitumikia vilabu mbalimbali ikiwemo Manchester United, Real Madrid, AC Milan, Beckham alikuwa mahiri kwa kupiga faulo na krosi kutoka winga ya kulia. Uwezo wake wa kufunga magoli ya faulo na kupiga krosi vilimjengea umaarufu mkubwa na kufanywa apendwe.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.