Mix

Utendaji wa Hospitali ya Ocean Road haujamridhisha Waziri wa Afya…maamuzi ya waziri yamefuatia

on

Kasi ya Rais Magufuli na kila serikali yake inachokifanya kwa sasa Waziri  wa Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imemsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk, Diwan Msemo ili kupisha uchunguzi  pamoja na mambo mengine ili kubaini mgongano wa kimaslahi ulioathiri utendaji wa taasisi hiyo chini ya kaimu mkurungenzi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu imesema kutokana na ziara alizofanya Dk.Rais MAGUFULI inaonyesha  kukosekana kwa dawa katika hospital za Serikali huku vituo vya afya binafsi vikiwa na dawa.

Taarifa ya Waziri hiyo imesema kuwa upungufu wa dawa umeendelea kujitokeza kwa karibu zaidi na baadhi ya wagonjwa walieleza kwa uchungu jinsi wanavyopata dawa kwa tabu  hatazile  wanazotakiwa wapate kwa bei ya ruzuku au zilezinatakiwa kutolewa bure na Serikali.

Bodi ya Taasisi ya Ocean Road imeagizwa kutafuta mtu atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi na Dk.Msemo anayefanyiwa uchunguzi.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

 

 

 

 

Tupia Comments