Leo August 14, 2018 tunayo story kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ambapo imetangaza kuwa na mfumo mpya wa kielektroniki utakomuwezesha mwanafunzi kuthibitisha chuo anachokwenda kusoma baada ya kuchaguliwa na zaidi ya chuo kimoja.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mtendaji TCU, Charles Kihampa amesema kutokana na kuwepo kwa malalakimiko TCU imeamua kutoa Code maalumu ya siri kwa wanafunzi watakao chaguliwa na zaidi ya chuo kimoja itakayo muwezesha kuthibitisha chuo au program anayotaka kusoma.
Kihampa amesema kuwa TCU itatuma SMS yenye namba hiyo maalumu ya siri ambayo itakuwa ni siti ya mwombaji pekee na atatakiwa kuitoa pale tu anapotaka kuthibitisha chuo anachotaka kusoma. “Tume itatoa muda maalumu kwa waombaji kuthibitisha chuo au programu ya masomo anayopenda.
Hata hivyo TCU imetangaza kufunga dirisha la maombi ya kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu la awamu ya kwanza ambalo liliansa Julai 20, 2018 ifikapo kesho Agost 15/8/ 2018. “Baada ya kufunga dirisha la udahili urodha ya waombaji itaidhinishwa na orodha ya seneti au bodi za kitaaluma zitawasilishwa TCU ili kuhakiki kama wahusika wanakidhi vigezo na baada ya TCU kuchagua orodha ya waombaji itawasilisha waombaji wenye sifa za kujiunga na vyuo,” amesema Kihampa.
Unaweza kutazama kwa kubonyeza link hii hapa chini……..
Hii ndio Dodoma bwana, laki tisa tu unapata kiwanja, Bonyeza link hapa chini kutazama