Leo May 22, 2019 Kesi ya kuwakata masikio ya kushoto watu wawili inayomkabili Mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha Aslim Minja imeahirishwa hadi June 21 mwaka huu kwenye Mahakama ya Wilaya ya Arumeru
Imedaiwa Mahakamani hapo kwamba Mtuhumiwa alitenda kosa hilo July 21, 2017 eneo la Njiro Jijini Arusha huku akijua kuwa ni kinyume cha sheria.
Watu wawili wanaodaiwa kutendewa matukio hayo ni Aloyce Petro na Samwel Sambeke ambao walikuwa wafanyakazi wake.