Mbunge wa Kawe Halima Mdee ameruhusiwa kutoka Hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe tumboni na amesema anaendelea vizuri huku akiwashukuru wote waliomuombea na kumtumia salamu za pole.
Mdee alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam tangu Alhamisi ya Juni 6, 2019.
HABARI za asbh Wakuu. Kwa heshima kubwa, naomba niwashukuru WOTE kwa MAOMBI na SALAMU za POLE. Nimeshatoka HOSPITAL na AFYA yangu INAIMARIKA kwa KASI ya AJABU. Sina cha kuwalipa kwa UPENDO wenu MKUU, Mungu AWASIMAMIE na KUWABARIKI katika KILA JAMBO MNALOLIFANYA. 🙏🏿 sana.
— Halima James Mdee (@halimamdee) June 10, 2019
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe nae akaandika kupitia ukurasa wake wa Twitter
Nilipata nafasi ya kumsabahi dada yangu na kamaradi wangu katika harakati za Ujenzi wa Demokrasia nchini Bi. @halimamdee ambaye ni mgonjwa kwa siku kadhaa sasa. Nashukuru Mola kuwa anaendelea vizuri na sasa ameruhusiwa kupumzika nyumbani. Namtakia kheri apone haraka pic.twitter.com/gmqiVS3G1I
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) June 9, 2019
MAGUFULI “HUYU MKURUGENZI ALIPIGA SIMU NIKAMTUKANA, KITU CHA AJABU KIPUMBAVU”