Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati ya upatikanaji wa vifaranga vingi vya samaki pamoja na chakula bora cha samaki sambamba na kuendelea kutoa elimu ya ufugaji ili wananchi waweze kufuga samaki kwa tija.
Akizungumza kwenye maonesho ya Nanenane Kitaifa Mkoani Simiyu, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amesema Serikali imelazimika kuweka mikakati hiyo kutokana na wananchi wengi kuwa na mwamko wa kufuga samaki kibiashara licha ya kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa vifaranga bora na chakula kwa bei nafuu.
“Kwa mfano mwaka jana uhitaji wa mbegu za samaki ulikuwa unafikia takriban samaki Milioni 40 lakini sisi tumeweza kuzalisha kama Milioni 18 kwa hiyo kuna mikakati ipo kuhakikisha vituo vya Serikali pamoja na kuhamasisha vile vya watu binafsi kuzalisha vifaranga bora.” Dkt. Tamatamah
ISAYA WA TABORA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO