Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu George Waitara amesema uanzishwaji wa Hifadhi mpya tano Mkoani Kagera utaleta fursa nzuri ya mazingira ya uwekezaji katika Sekta ya Utalii nchini huku akiridhishwa na mazingira rafiki yaliopo katika Hifadhi hizo.
Waitara amezungumza hayo mara baada ya kutembelea Hifadhi hizo za Biharamlo, Burigi na Kimisi zinazojulikana kama BBK na Rumanyika zilizoko Mkoani Kagera misitu ambayo ilikuwa mapori ya akiba ya Ibanda, Rumanyika na Biharamlo ambayo Serikali imeyapa hadhi ya kuwa Hifadhi za Taifa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Jenerali Mstaafu Geprge Waitara amesema Hifadhi hizo zitaleta fursa ya ukanda huo kufunguka zaidi katika suala utalii na kusema wataendelea kuwekeza katika kuhakikisha maeneo hayo yanafikika.
Martin Loibooki ni Kamishina wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi pamoja na Mshauri wa Masuala ya Utalii Shirika la Hifadhi TANAPA Ibrahim Mussa amezungumzia umuhimu wa Hifadhi hizo na mipango ya uendelezaji miundiombinu.
ANG’ATWA APATA KIDONDA CHA AJABU HAKIPONI MWAKA WA 13, USIKU JAMAA ADAI ANABADILIKA KUWA MNYAMA