Michezo

Maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Simba SC dhidi ya Mzee Kilomoni

on

Leo August 13, 2017 Simba SC imefanya Mkutano Mkuu wa Wanachama katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo moja ya makubaliano yaliyofikiwa na wanachama ni kumuondoa Mzee Kilomoni kwenye Bodi ya Wadhamini wa Klabu hiyo.

Mbali na kumuondoa kwenye Bodi ya Wadhamini, Klabu ya Simba imemsimamisha uanachama na itamuandikia barua rasmi kwa ajili ya kumpa nafasi ya kujitetea.

Aidha, Mkutano huo umemchagua Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Adam Mgoi kuchukua nafasi ya mzee Kilomoni huku Prof. Juma Kapuya akipitishwa kuwa Mdhamini kuchukua nafasi ya marehemu Ally Klaiyst Sykes.

ULIPITWA? Bodi ya Wadhamini ya Simba SC baada ya kufungua kesi…PLAY kwenye hii VIDEO kutazama!

KAMA ULIPITWA…play kwenye video hii kujua Maamuzi ya Mahakama ya Kisutu kuhusu mkutano wa Simba SC August 13!!!!

Soma na hizi

Tupia Comments