Staa wa soka wa kimataifa wa Senegal anayeichezea Liverpool ya England Sadio Mane leo Jumanne ya April 11 2017 amefanyiwa upasuaji wa goti lake la kushoto.
Mane ameonekana mchana wa leo akitoka katika hospital binafsi jijini London kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kushoto licha ya kuwa Liverpool walikuwa na matumaini ya staa wa kutofanyiwa upasuaji.
Upasuaji huo sasa utamuweka nje ya uwanja Sadio Mane kwa wiki nane kwa lugha rahisi staa huyo wa Liverpool ndio amemaliza kuitumikia Liverpool msimu huu kutokana na jeraha hilo.
VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera April 2 2017