Mtu unaweza kutarajia kuona maji ya bahari yamapokutana, yatachanganyika na maisha kuendelea kama kawaida. lakini hiyo si kwa Bahari ya Pacific na Atlantic, zenyewe maji yake hayachanganyiki kila upande yanabaki kama yalivyo na kuishia hapo hapo yanapokutania, huko Alaska Marekani.
Wanasayansi wanasema hii kitu inatokana na asili ya Bahari hizi japo zote ni bahari lakini maji yake yana sifa tofauti.
Tofauti katika uzito wa maji haya, joto na uchumvichumvi wa barafu yaliyoyeyuka ya maji haya pamoja na maji ya ufukweni mwa ghuba ya Alaska, ndivyo vinavyosababisha yashindwe kuchanganyikana.