Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Chama hicho kipo na kitaendelea kuwepo, akisisitiza “ACT is here to stay”
Amesema, “Nguvu za ACT-Wazalendo si silaha wala mabomu bali ni Umoja wa Wanachama wake na mshikamano ambapo upo katika Chama”.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa, kwa ufahamu wake, yeye ana jukumu la kutekeleza ambayo yameamuriwa kwenye vikao vya kitaifa na atasimamia katika hilo.
Aidha, amezungumzia suala la baadhi ya Vijana katika Chama hicho kusema anataka king’ora tu amesema, vijana hao wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kulinda maamuzi ya Chama.