Moto umezuka katika Shule ya African Muslim iliyopo Moshi Mjini Mkoani Kilimanjaro na kuteketeza mabweni ya Wanafunzi yatima, moto huo ambao bado haujajulikana chanzo chake ulianza majira ya Saa 1 kasoro ambapo Wanafunzi wote walikua katika ukumbi wa kulia chakula hivyo haukuleta madhara kwa Mwanafunzi yeyote yule zaidi ya kuharibika kwa vitu vyao.
Mkuu wa Wilaya Alhaj Rajab Kundya ametoa pole kwa Wanafunzi hao na kuwaahidi Serikali itafuatilia jambo hilo kwa umakini na kuweza kubaini chanzo cha moto huo na endapo itagundulika kuna yeyote aliyehusika na moto huo atachukuliwa hatua kali za kisheria.