Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amewafungia kwa muda wa miezi mitatu Madereva 10 wa Mabasi ambao wamekuwa wakikiuka Sheria ya Usalama Barabarani kwa kuendesha kwa mwendokasi.
Simbachawene ametoa kauli hiyo Dodoma ambapo ameliagiza pia Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kuwachukulia hatua Madereva hao ikiwa ni pamoja na kuwapeleka Mahakamani kwa makosa hayo.
Waliofungiwa ni Madereva wa Mabasi ya Kampuni za Kimotco (Arusha- Musoma), Al Saedy (DSM- Kilombero), MB Coach (DSM – Arusha), Baraka Classic (DSM – Masasi), Maning Nice (DSM – Tunduma), Machinga (DSM-Mtwara), Ester Luxury (DSM- Moshi), NBC Classic (Tabora – Kigoma), Kilimanjaro Express (DSM- Arusha) na Kapricon (DSM – Moshi)
“Kwa Mamlaka niliyonayo nawafungia Madereva hawa kwa muda wa miezi mitatu, nawaagiza Wamiliki wa Mabasi haya ambayo Madereva wamekiuka Sheria ya Usalama Barabarani kuhakikisha wanachukua hatua stahiki kwa Madereva wao”———Waziri Simbachawene.