Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslimu, amesema kuwa madereva wawili wa mabasi ambao video yao ilisambaa mitandaoni wakishindana barabarani, atawachukulia hatua za kuwaondolea sifa za kuendesha magari hayo, kuwafungia kwa miezi 6 pamoja na kuwapeleka mahakamani.
“Nimechukua hatua kali sana, tumewakamata wote na wako ndani na tumeandaa utaratibu wa kisheria ikiwemo kuwafikisha Mahakamani’ Kamanda Muslim
Sheria inanipa uwezo wa kuwaondolea sifa wa kuendesha haya magari ya mizigo na biashara na kwa miezi 6 hawa hawatokuwa barabarani wakiendesha Mabasi wala Malori labda hivi vigari vidogo” Kamanda Muslim
Juzi ilisambaa video mitandaoni ikionesha Madereva wa Mabasi wakikimbizana barabarani bila kujali usalama wao wala abiria waliokuwa nao.
BABA WA MWANAFUNZI ALIEUAWA KISA MAPENZI CHUONI AONGEA “NDIO MSOMI PEKEE KWETU, TULITAKA ATUTUNZE”