Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la HabariLEO yenye kichwa cha habari ‘Magufuli hajazuia siasa’
#HabariLEO Msajili vyama vya siasa asema Rais hajazuia siasa bali alichokitaka ni ushirikiano kutoka kwa wanasiasa pic.twitter.com/kgDWtTy3m9
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
Gazeti la HabariLEO limeripoti kuwa Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametetea kauli ya Rais John Magufuli kuhusu kufanya siasa wakati huu na kwamba alichotaka kiongozi huyo wa nchi ni ushirikiano kutoka kwa wanasiasa wenzake ili kuwaletea maendeleo kwa wananchi.
Kupitia gazeti hilo amesema Rais Magufuli katika kauli yake ile hakumaanisha kuzuia shughuli za siasa nchini isipokuwa alielezea kuwa hatakuwa tayari kuona siasa nchini zinakwamisha mikakati ya kuwapeleka wananchi maendeleo yao.
Gazeti hilo limemnukuu Jaji Francis Mutungi ambapo amesema……>>>‘watu wameitafsiri tofauti kauli ya Rais Magufuli, lakini ni kwamba alikua akiomba ushirikiano na wanasiasa wenzake na wadau wote wa siasa kuleta maendeleo, kwa hiyo kabla ya kukosoa kauli ni vyema ukafanya utafiti siyo kuibeba na kuitafsiri kwa mrengo tofauti’
Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kwenye magazeti ya leo June 25 2016
#MWANANCHI Mbowe asema hawatakubaliana na kauli ya JPM ya kukataza mikutano ya shughuli za siasa hadi mwaka 2020 pic.twitter.com/zFjPTvq3Xw
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
#MWANANCHI Uhakiki mpya Mwanza umebaini watumishi hewa 1,057 na wameiingizia Serikali hasara ya bil 2.1 pic.twitter.com/k0sdW2bulA
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
#MWANANCHI Licha ya kukataa kuhusika kumvua kofia mbunge Mlinga, Theonest amebainika kufanya kosa na kupewa onyo pic.twitter.com/K7hTSeKzOW
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
#NIPASHE Watumishi 400 kati ya 597 NIDA waliosimamishwa kazi wamelipwa madai ya malimbikizo ya mishahara yao pic.twitter.com/60LB6MYisQ
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
#NIPASHE UDSM imetangaza kuanza kutumia kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano chuoni hapo pic.twitter.com/D0xLRfPpJg
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
#NIPASHE Baadhi ya walimu Shule ya msingi Tinai, Dodoma wamekimbia kutokana na vitendo vya kishirikina pic.twitter.com/CaRKajCs12
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
#HabariLEO Zaidi ya wanafunzi 90,248 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi mwaka 2016 pic.twitter.com/hRT5fRdZld
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
#MTANZANIA Utaratibu mpya wa kulipia chakula Muhimbili hautaihusu MOI, wagonjwa wataendelea kupelekewa chakula pic.twitter.com/hXLkuei7dt
— millardayo (@millardayo) June 25, 2016
ULIKOSA KUANGALIA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNE 25 2016 AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HAPA CHINI?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE